FAO yaahidi kuunga mkono juhudi za Tanzania
18 October 2023, 9:29 am
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama, viongozi wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Na Mindi Joseph.
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa amesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limeahidi kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania katika kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo.
Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zina mipango ya kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula ndani ya nchi na ziada kuuza nje ifikapo 2030.
Waziri Mkuu ameyasema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza jana Oktoba 16 hadi Oktoba 20, 2023.
Awali, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alisema serikali imeendelea kuwashawishi vijana kushiriki katika shughuli za kilimo kwani mbali na kuongeza uzalishaji wa chakula, pia kilimo ni miongoni mwa sekta zinazotoa ajira nyingi, hivyo watakuwa wamejihakikishia ajira.