Zaidi ya wananchi 1500 wafikiwa na elimu ya malezi
15 September 2023, 7:12 am
Program jumuishi ya malezi, makunzi na maendeleo ya awali ya mtoto ilizinduliwa mwaka 2021 na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ambapo wadau mbalimbali wanatekeleza program hiyo.
Na Mariam Matundu.
Zaidi ya wananchi elfu moja na mia tano wamefikiwa na elimu ya malezi na makuzi ya mtoto katika utekelezaji wa program jumuishi ya malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto mkoa wa Dodoma.
Akizungumza na taswira ya habari mtaalamu wa jinsia kutoka taasisi ya Action for community care Stella Matemu amesema mafanikio hayo yamekuja kutoka na afua mbalimbali zinazotekelezwa na wadau wanaotekeleza program hiyo.
Aidha amesema kwasasa wameanza zoezi la kutambua watoto wenye ulemavu katika wilaya zote za Dodoma kuanza mwaka 0 hadi miaka 8 ili kuhakikisha kundi hili pia linapata haki ya kupata elimu.
Nae afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Dodoma Honoratha Rwegasira amesema kuwa program hiyo ni jumuishi na kuwataka wazazi kutowabagua watoto wenye ulemavu .