Umaskini watajwa kuchangia lishe duni
16 August 2023, 5:09 pm
Lishe ni muhimu kwa afya ya Watoto na Watu wazima ambapo ulaji duni kwa Watoto unaweza kusababisha mashambulizi ya maradhi kama vile utapiamlo na udumavu wa mwili.
Na Yussuph Hassan.
Ukata wa Maisha pamoja na Elimu duni kwa baadhi ya Watu imeendelea kuwa moja ya changamoto katika kuzingatia lishe bora.
Lishe ina uhusiano mkubwa na afya, lishe bora hufanya mwili kukuwa vyema na kuulinda dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Hivi karibuni Nchini kumekuwa na ongezeko la magonjwa yasio ya kuambukizwa yanayotokana na ulaji usiofaaa, baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wanabainisha nini sababu ya baadhi yao kutozingatia lishe bora.
Aidha wameomba Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya kuzingatia lishe bora na mlo kamili.
Kwa upande Afisa lishe kutoka Dodoma Neema Chaula amesema kuwa lishe bora haihitaji gharama kubwa isipokuwa jambo la msingi ni Watu kuzingatia mpangilio wa vyakula.