Wadau wa mazingira watakiwa kuanza kuandaa vitalu vya miti
28 July 2023, 1:11 pm
Ama kweli penye nia pana njia haijalishi ni kianganzi ama masika lakini zoezi la upandaji miti limeendelea kufanyika.
Na Mindi Joseph.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amewaomba wadau wa mazingira kuanza kuandaa vitalu vya upandaji miti kwa msimu wa mvua unaokuja.
Shekimweri amewaongoza wadau wa mazingira kupanda miti 200 katika shule ya sekondari Lukundo ambapo zoezi hilo limeratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Green Home.
Mkuu wa shule ya sekondari Lukundo ameomba kujengewa uzio ili kulinda miti iliyopandwa na kwa usalama wa wananfunzi huku mkurugenzi wa shirika la Green Home akibainisha lengo la shirika hilo kupanda miti ndani ya shule hiyo ya sekondari.
Wanafunzi wanasema ni faraja kwao kuona miti inapandwa katika shule yao.
Shule ya Sekondari Lukundo ina jumla ya wanafunzi 1365.