Serikali yatakiwa kuhamasisha vijana kujikita katika kilimo
26 July 2023, 5:42 pm
Kartika kupunguza changamoto ya ajira na ugumu wa maisha kwa vijana nchini serikali imeendelea kusisitiza juu ya suala la kilimo biashara kwa kuanzisha programu mbalimbali kwa lengo la kuwawwezesha kujikwamua kiuchumi ikiwa ni katika kuanzisha mashamba ya kilimo pamoja na masoko.
Na Thadei Tesha.
Ili kuwasaidia vijana wengi kunufaika na fursa zinazotokana na kilimo serikali imetakiwa kuendelea kuweka nguvu zaidi ili kuwahamasisha vijana wengi kujihusisha na miradi ya kilimo kwani imekuwa na kasi kubwa ya kutoa ajira kwa vijana.
Dodoma tv imefanya mahojiano maalum na mkurugenzui wa shirika la VALUES OF YOUTH ENTERPRENUERSHIP AND ECONOMIC GROWTH VYEEG Ndugu Jofrey Sanga ambapo hapa anasema kuwa kupitia shirika hilo wameendelea kutoa elimu na ujuzi kwa lengo la kuwasaidia vijana kujiingiza katika kilimo biashara.
Lakini je muamko wa vijana kujiingiza katika fursa hiyo upoje kwa sasa hapa anabainisha.