Viongozi wa kijiji Zejele watakiwa kuacha kujihusisha na uuzaji wa maeneo
21 July 2023, 4:11 pm
Mhe Nolo amesema kuwa serikali ya kijiji isijiingize kwenye udalali wa kuuza ardhi kwani itakuwa ni chanzo cha mgogoro kwa wananchi .
Na Seleman Kodima.
Viongozi wa serikali ya kijiji cha Zejele kata ya Nondwa wametakiwa kuacha kujihusisha na uuzaji wa maeneo ili kuepukana na migogoro ya ardhi.
Wito huo umetolewa na mbunge wa Bahi Mhe. Keneth Nolo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji zejele katika mkutano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa Bahi.
Aidha amewataka viongozi wa serikali ya kijiji kuwatetea wananchi maana wana wajibu wa kuwatumikia wananchi ambao wamewapa mamlaka ya kuwaongoza.
Wakati huohuo amezungumzia mpango wa serikali wa ujenzi barabara ya Bihawana, Chali, Chifutuka hadi Sanza Manyoni kwa kiwango cha lami na kuwahakikishia wananchi wa Zejele kujiandaa kwa ajili fursa ya uwepo wa barabara hiyo katika kujiletea maendeleo yao.