Makatibu tawala watakiwa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia utawala bora
4 July 2023, 6:11 pm
Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Ungozi yamehusisha Makatibu Tawala wa Wilaya 135 za Tanzania Bara.
Na Mindi Joseph.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Makatibu Tawala wa Wilaya zote Tanzania Bara watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia utawala bora, miiko na maadili ya viongozi wa umma.
Ametoa maagizo hayo leo Jumanne, Julai 04, 2023 wakati akifungua semina elekezi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema lengo ya mafunzo hayo ni kuongezea weledi kwa viongozi hao ili kuimarisha utawala bora.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angela Kairuki amewataka viongozi hao watimize majukumu yao ipasavyo na wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa maagizo ya viongozi katika maeneo yao ya kazi.