Vijana watakiwa kutumia fursa zinazojitokeza kujikwamua kiuchumi
22 June 2023, 5:01 pm
Shirika la Kingdom Leadership Network Tanzania(KLNT) limekuwa likiratibu mikutano ya maombi kwa Taifa ikifahamika kama Tanzania Prayer Breakfast.
Na Rabiamen Shoo.
Wananchi hususan vijana wametakiwa kuzitumia vizuri fursa zinazojitokeza katika maeneo yao kupata elimu hususan namna ya kufanikiwa kiuchumi.
Wito huo umetolewa hii leo jijini Dodoma na mwenyekiti mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali la KLNT Bw.Isaac Mpatwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.
Mpatwa amesema kuwa mbali na mkutano huo kuwa wa fursa kwa vijana lakini utakuwa na malengo mengine matatu.
Aidha Mpatwa amesema kuwa kutakuwa na wanenaji kutoka ndani na nje ya nchi ambao anawataja:
Katika mkutano huo Bilionea kutoka nchini Marekani Llyod Ward atakuwa akiwafundisha vijana namna ya kufanikiwa katika shughuli zao zikiwemo kibiashara kama anavyosema Geofrey Simbeye ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa Taasisi ya sekta binafsi TPSF ambae pia ni Mkurugenzi mkazi wa Ward Holdings International.
Naye mchungaji Dr.Canon Mosses Matonya ambaye ni katibu mkuu wa baraza la Kikristo Tanzania amesema kuwa kinachotakiwa ni elimu ya kutosha ili kupata maarifa ya kutawala na kutunza vitu vyetu.