Vijana Kikuyu waipongeza serikali kuwasogezea huduma, elimu ya Afya
16 June 2023, 2:28 pm
Katika kata ya Kikuyu Kaskazini watu 103 wamepata elimu na kupima masuala ya lishe ambapo asilimia 12.6% walibainika na utapiamlo, watu 80 wakipata elimu juu ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza na Bonanza hilo linatarajiwa kuhitimishwa siku ya kesho Jumamosi Makulu.
Na Mindi Joseph.
Baadhi ya vijana katika kata ya Kikuyu Kaskazini jijini Dodoma wameipongeza Wizara ya Afya kwa kuwasogezea huduma na elimu ya afya kupitia Afya Bonanza.
Vijana hao wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Taswira ya habari katika mwendelezo wa Afya Bonanza kata ya Kikuyu.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya vijana Halmashauri ya Jiji la Dodoma Daniel Mfungo Manyama amesema Bonanza la Afya katika mkoa wa Dodoma lililoandaliwa na Wizara ya Afya lina umuhimu mkubwa kwa ajili ya vijana kutambua afya zao.