Vituo vya afya vyatakiwa kununua majokofu ya kuhifadhia mazao ya damu
14 June 2023, 6:00 pm
Tanzania leo imeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya Wachangia Damu Duniani ambayo inalenga kuongeza ufahamu na kuwashukuru wafadhili wa damu wa hiari, wasiolipwa kwa zawadi zao za kuokoa maisha.
Na Mindi Joseph.
Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu ametaka vituo vyote vya afya vya serikali nchini kununua majokofu ya kuhifadhia mazao ya damu.
Waziri Ummy ameyasema hayo katika uzinduzi wa huduma za damu salama kituo cha Kanda ya Kati Dodoma siku ya wachangia Damu Duniani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amesema uchache wa vituo umechangia kutotengeneza mazao ya damu.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Dk. Neema Kileo anaainisha kuwa utafiti unaonesha kuwa vifo 43 kati ya 100 vinasababishwa na wanawake kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua.