Serikali yataka mapendekezo sheria ya sauti zinazozidi katika nyumba za ibada
13 June 2023, 12:39 pm
Kongamano hilo lina lengo la kujadili na kuwajengea uelewa viongozi wa madhehebu ya dini nchini juu ya kufahama athari zinazoweza kutokana na kelele na mitetemo katika nyumba za ibada ili wakawe mabalozi kwa waumini wao.
Na Fred Cheti.
Serikali imewataka viongozi wa madhehebu yote ya dini kupitia jumuiya ya Maridhiano ya amani nchini (JMAT) kwa kushirikiana na NEMC kufanya mapitio ya sheria la suala la sauti zinazozidi katika nyumba za ibada na kutoa mapendekezo yao.
Maagizo hayo yametolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa wakati akifungua kongamano la kitaifa la kujengewa uelewa kwa viongozi wa dini juu ya athari za sauti zilizozidi katika jumba za ibada lililoandaliwa na Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na jumuiya ya Maridhiano ya Amani nchini (JMAT)
Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Jaffo anaelezea azma ya serikali katika jambo hilo.
Nae Mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya Maridhiano ya amani nchini (JMAT)Dkt.Alhad Mussa amezungumzia malengo ya jumuiya hiyo kwa kushirikaina na serikali katika jambo hilo.