Berege: Madereva malori wapatiwe elimu ya kujilinda dhidi ya kemikali
25 May 2023, 7:10 pm
Ameiomba serikali kutumia nguvu kubwa ya kulinda sekta ya uchukuzi Ili iendelee kuajiri madereva.
Na Fred Cheti.
Wito umetolewa kwa wamiliki wa malori nchini kuhakikisha madereva wao wanapewa elimu kwa ufasaha Ili waweze kujilinda na wasipate madhara wakati wa usafirishaji wa kemikali.
Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri Bi.Pendo Berege ametoa wito huo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya madhara ya kemikali kwa viongozi wa vyama vya madereva katika ukumbi wa jengo la mkemia mkuu wa serikali jijini Dodoma.
Aidha Bi. Berege amesema matarajio yake baada ya mafunzo hayo madereva wataweza kuzingatia taratibu za kisheria za utoaji wa taarifa zinazohusiana na masuala ya sumu na kemikali na pia watazingatia usafirishaji salama wa kemikali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha madereva Tanzania (TADWU) Bw. Schubert G. Mbakizao amesema wao kama viongozi wa madereva kazi yao ni kuhakikisha kwamba wanalinda vyanzo ambavyo vinaweza kusapoti serikali iweze kuviendeleza hususani kwenye bandari.