Rais Samia awataka wazazi, walezi kuimarisha malezi kwa watoto
20 August 2024, 5:27 pm
Picha ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Skuli ya Maandalizi Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi katika eneo la Makunduchi, Unguja, Zanzibar .Picha na Ikulu.
Uimarishaji wa malezi ya mtoto katika siku 1000 ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Afya na Uzazi Bora.
Na Pius Jayunga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi nchini kuimarisha malezi ya mtoto katika siku 1000 tangu kuzaliwa kwake ikiwemo afya bora pamoja na maadili katika jamii.
Ametoa wito huo katika hafla ya uzinduzi wa Skuli ya Maandalizi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Watoto wa Shehia ya Tasani Makunduchi Zanzibar kuekelea kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais Dkt. Samia amesema uimarishaji wa Malezi ya Mtoto katika siku 1000 ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Afya na Uzazi bora.
Katika hatua nyingine Rais Samia amezipongeza Taasisi zinazounga Mkono Kampeni ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia ikiwemo kituo hicho.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Reila Mohamed Musa amesema Serikali inatarajia kujenga Skuli za maandalizi zipatazo 33 ikiwani utekelezaji wa Sera ya Elimu ya maandalizi kuwa lazima Visiwani Zanzibar.