Wakazi wa Dodoma waaswa kuacha kuchimba mchanga katika viwanja vya watu
15 March 2022, 1:52 pm
Na; Neema Shirima.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Dodoma wenye tabia ya kuchimba mchanga katika viwanja vya watu wametakiwa kuacha tabia hiyo kwani watachukuliwa hatua kali mara tu watakapokamatwa wakifanya vitendo hivyo
Hayo yamesemwa na Afisa mazingira mkoa wa Dodoma Bwn Dikcson Kimaro wakati akiongea mbele ya mkuu wa mkoa katika ziara aliyoifanya katika kata ya Iyumbu ambapo amesema endapo mtu atabainika katika uchimbaji wa mchanga atachukuliwa hatua kali za kisheria
Amesema ni vema kutii sheria bila shuruti kwani iwapo mtu hatotii agizo hilo atapelekwa katika wizara ya madini ambapo wao faini yao ni shilingi milioni moja na nusu
Amesema kwa yoyote atakaewafichua wahalifu wa viendo hivyo watapewa zawadi ya nusu ya faini ya mhalifu huyo
Ni jukumu la kila jamii kushiriki katika kutunza mazingira ili kuepuka ukame pamoja na majanga mbalimbali ikiwemo mmomonyoko wa ardhi