Rais Samia asema bado kuna malalamiko mengi ya wananchi juu ya ucheleweshwaji wa haki
2 February 2022, 3:53 pm
Na; Pius Jayunga.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samia suluhu Hassan amesema bado kuna malalamiko mengi ya wananchi juu ya ucheleweshwaji wa haki katika muhimili wa mahakama.
Rais samia ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria Nchini ambayo yamefanyika katika viwanja vya chinangali park jijini Dodoma.
Amesema yapo malalamiko ya wananchi kucheleweshewa haki na hata kunyimwa haki zao ikiwemo wanawake wajane pamoja na migogoro ya ardhi.
Amewataka watendaji wa mahakama kutenda haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi ikiwemo baadhi ya wananchi kushindwa kuweka wakili katika usimamizi wa kesi yake.
Kwa upande wake Jaji mkuu wa Tanzania profesa Ibrahimu Juma amesema mfumo wa mahakama mtandao ni lazima uende sambamba kwa kuwashirikisha wananchi ili kuongeza ufanisi.Clip 3 Juma ……………..
Akizungumzia utaratibu wa utungaji wa sheria bungeni unaoshirikisha wananchi, spika wa bunge Dr. tulia ackison amesema.
Clip 4 Tulia………………..
Kilele cha maadhimisho siku ya sheria nchini kimefanyika katika vijana vya chinangali park jijini Dodoma mgeni rasmi akiwa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. samia sulu Hassan huku kaulimbiu ya maadhimisho hayo ikisema zama za mapinduzi ya nne ya viwanda safari ya maboresho kuelekea mahakama mtandao.