Serikali imetakiwa kuwakea mazingira mazuri ya kujinzia wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia ili waweze kufanya vizuri
29 July 2021, 10:05 am
Na;Mariam Matundu .
Ili kuondoa changamoto za kujifunza kwa wanafunzi Viziwi imeshauriwa kuwekewa mazingira mazuri ya kujifunzia ikiwemo kutungiwa mitihani yao maalumu katika baadhi ya masomo tofauti na wanafunzi wasio viziwi .
Hayo yameelezwa na mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule ya msingi Dodoma viziwi Leah Mlayi ambapo amesema zipo mbinu za ufundishaji ambazo haziwezi kutumiwa na mwalimu anaefundisha wanafunzi viziwi hivyo baadhi ya mambo inakuwa ngumu kwa mwanafunzi kuelewa.
Amesema katika mitihani mbalimbali yapo baadhi ya maswali ambayo yanahitaji mwanafunzi ajieleze ambapo inakuwa ngumu kwa mwanafunzi kiziwi kwani mambo mengi anakuwa hashirikishwi hivyo kusababisha kukosa maksi katika maswali hayo.
Nae mshauri mwelekezi wa haki elimu Wilbaforce Meena amesema ili kubadilisha mambo yote ni muhimu kufanyika mabadiliko ya sera ya elimu hasa katika mitaala na suala la upimaji katika mitihani.
Kwa upande wake afisa elimu elimu maalumu jiji la Dodoma Agnesi Mwingila amesema wanaendelea kuiomba serikali kubadili sera na kuwapima wanafunzi kulingana na mahitaji yao .