Mlowa bwawani yatarajia kutoa elimu kwa wananchi wake juu ya kujikinga na virusi vya korona
24 June 2021, 10:53 am
Na; Benard Filbert.
Uongozi wa kata ya Mlowa bwawani hii leo unataraji kukutana na wananchi wa eneo hilo ili kuwapatia elimu pamoja na kuwahimizi kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vinavyo sababisha homa ya mapafu.
Hayo yameelezwa na diwani wa kata hiyo wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amesema kuwa virusi vinavyosababisha homa ya mapafu ni hatari kwa kila mtu hivyo tahadhari zinahitajika kuchukuliwa.
Amesema katika kuchukua tahadhari zaidi leo kutakuwa na mkutano wa hadhara ili kuwahimiza wakazi wa kata hiyo kuchukua tahadhari na kuzingatia vitu muhimu vitakavyo wasaidia kupambana na homa hiyo.
Amesema hivi sasa wameanza kusisitiza taasisi mbalimbali ambazo zinamuingiliano wa watu katika kata hiyo kuhakikisha wanaweka vifaa vya kunawia maji ili kila mmoja afuate taratibu kulingana na maelekezo ya wizara ya afya..
Kufuatia kuendelea kwa mambukizi ya ugonjwa wa corona nchi mbali mbali serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia kwa waziri wa afya ustawi wa jamii wazee jinsia na watoto mh Nassor Ahmed Mazrui alinukuliwa akisema wamepokea taarifa kutoka kwa vyanzo mbali mbali juu ya uwepo wa wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona.
Wananchi wanahimizwa kuendelea kuchukua tahadhari ikiwepo kuvaa barakoa pamoja na kunawa kila mara ili kuepuka maambukizi ya homa ya mapafu.