Dodoma FM

Uhaba wa Alizeti wachangia mafuta ya kula kupanda bei

23 April 2021, 10:42 am

Na; SALIM KIMBESI.

Wafanyabiashara wa mafuta ya kupikia katika soko la Majengo jijini Dodoma wamesema kuwa uhaba wa zao la alizeti ndio umechangia bei ya bidhaa hiyo  kupanda.

Wakizungumza na Dodoma Fm baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa, upatakanaji wa alizeti umekuwa mgumu tofauti na msimu uliopita ambapo ilipatikana kwa wingi.

Hata hivyo wamesema zao wanatarajia bei ya mafuta hayo kushuka baada ya mavuno ya alizeti katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma.

Nao wanunuzi na watumiaji wa mafuta ya alizeti wamesema kuwa wengi wao wanashindwa kumudu bei kutokana na bei kubwa, ambapo wameiomba Serikali kulitazama vema jambo hili, kwa sababu linawapa changamoto.

Mafuta ya alizeti yamekuwa yakipatikana kwa wingi kila inapofika msimu wa mvuno ya zao la alizeti ambapo hali hiyo huchangia pia kushuka bei.