Naibu PM azindua mwongozo usimamizi wa huduma za majitaka, tope kinyesi
20 August 2024, 6:31 pm
Picha ni Mwakilishi wa Mgeni Rasmi katika kongamano la kwanza la kitaifa la Usafi wa Mazingira 2024 ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu) William Lukuvi. Picha na Selemani Kodima.
Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Afya wameendelea na utekelezaji wa kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira yenye lengo la kuonesha umuhimu wa usafi kwa mtu binafsi.
Na Selemani Kodima.
Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amezitaka mamlaka za serikali za mitaa, sekta binafsi, wizara zenye dhamana ya usafi wa mazingira Ziruwasa , NEMC pamoja na wadau wengine kushirikiana kutekeleza malengo ya mwongozo wa usimamizi wa huduma za majitaka na tope kinyesi .
Agizo hilo limetolewa na Mwakilishi wa Naibu Waziri Mkuu ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu) William Lukuvi kuwa leo katika Kongamano la Kwanza la kitaifa la Usafi wa Mazingira lililoenda sambamba na uzinduzi wa muongozo wa usimamiz wa huduma za majitaka na tope kinyesi na mfumo ulioboreshwa wa uwasilishaji wa taaarifa za mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira kwa lugha ya kiswahili .
Akitoa msisitizo Naibu waziri Mkuu amewataka wadau wanaohusika katika kudhibiti na utoaji wa huduma za usafi wa mazingira waendelea kuimarisha ushirikiano .
Awali Waziri wa Maji Juma Aweso amezikumbushwa Mamlaka za maji safi na Usafi wa mazingira nchini kuhakikisha zinazingatia matakwa ya muongozo huo .
Ikumbukwe kuwa Wizara ya Maji kwa kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI ,Wizara Elimu ,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya afya wameendelea na utekelezaji wa kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira yenye lengo la kuonesha umuhimu wa usafi kwa mtu binafsi.