Dodoma FM
Kofia zinazotengenezwa kwa mkono na wakazi wa Kondoa
12 August 2024, 3:37 pm
Mzee Rofati anasema kazi hii ya utengenezaji wa kofia aliirithi kutoka kwa wake walio kuwa wanatengeneza hapo zamani.
Na Yussuph Hassan.
Leo katika kipindi cha Fahari ya Dodoma tunazungumzia umaarufu wa kofia zinazotengenezwa kwa mkono tangu miaka ya 50, kofia hizi zina umaarufu mkubwa ndani ya wilaya ya Kondoa na nje ya wilaya hii ambapo historia inaeleza kuwa kofia hizi zilikuwepo tangu enzi za ukoloni.
Mzee Rofati mwenyeji wa wilaya ya Kondoa anasema ameanza kazi ya kutengeneza kofia hizi tangu mwwaka 1970 na hapa anaeleza namna kofia hizi zinavyotengenezwa.