UCSAF yatakiwa kuvifikia vijiji ambavyo havina mawasiliano
25 April 2024, 6:26 pm
Ujenzi wa Jengo la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF ulianza April 2021 na ujenzi huu umegharimu bilion 3.8.
Na Mindi Joseph.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameitaka UCSAF kusimamia kwa karibu ujenzi wa minara ya mawasiliano unaoendelea na kuhakikisha vijiji ambavyo havina huduma ya mawasiliano ya simu vinapata huduma hiyo.
Dkt Mpango ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa jengo la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF amesema wananchi wanayo haki ya kupata mawasiliano ya uhakika ili waweze kushiriki katika shughuli za uzalishaji.
Watanzania zaidi ya milion 36 wanauwezo wa kupata mawasiliano huku simu janja kutosambaa vya kutosha ikitajwa kuwa changamoto na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye anabainisha hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule anasema kupitia ujenzi wa minara 77 katika kata 68 Wananchi Laki 750 ambao wana uhakika wa kupata mawasiliano.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Justina Mashiba anasema zaidi ya minara 100 imeshakamilika nchini