Wakazi wa Ilangali waiomba serikali kuboresha machimbo ya Madini
12 May 2023, 3:19 pm
Wananchi hao wameiomba Serikali kuyatazama machimbo hayo kwa jicho la tofauti ili yaweze kuwa msaada mkubwa wa kutatua changamoto mbalimbali za kijiji hicho.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Ilangali Kata ya Manda wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuboresha machimbo ya madini yaliyopo ndani ya Kata hiyo.
Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya Wananchi wamesema kuwa licha ya uwepo mgodi huo wa madini ya dhahabu kwa takribani miaka ishirini lakini bado kijiji chao hakijanufaika kwa ujumla kwani kimeendelea kukabiliwa na adha ya kukosekana kwa huduma mbalimbali za kijamii
Mwenyekiti wa kijiji cha Ilagali Bw.Anania Ngobingoa amesema kuwa kutokana na wachimbaji wa mgodi huo kukosa dhana za kisasa katika shughuli hiyo imekuwa ngumu kuzalisha pato la kuinufaisha jamii ya eneo hilo
Ngobingo ameiomba Serikali kufanya utafiti na usimamizi wa mgodi huo ili wananchi wa kijiji cha Ilangali waweze kunufaika na pato linalo patikana kwa wachimbaji hao
Naye Diwani wa Kata ya Manda Bw.Fedrick Mandyamba amekiri uwepo wa mgodi huo kwa muda mrefu ambapo hata hivyo hakuna mafanikio makubwa kwa jamii yaliyo tokana na uchimbaji wa dhahabu