Wahitimu wa mafunzo SIDO watakiwa kuzalisha bidhaa bora
25 April 2023, 12:43 pm
Awali kulitanguliwa na mafunzo y utengenezaji Sabuni na Batiki kama anavyobainisha Mkufunzi wa mafunzo hayo.
Na Alfred Bulahya.
Zaidi ya wahitimu 350 wa mafunzo ya usindikaji wa Vyakula na matunda wamehitimu mafunzo hayo yanayotolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO huku wakitakiwa kuhakikisha wanakwenda kutengeneza bidhaa bora.
Mafunzo hayo yaliyodumu kwa kipindi cha Siku Nne yamehusisha wanachaama kutoka Taasisi ya Wanawake na Uchumi wa Viwanda WAUVI ambao wamepata elimu ya namna ya kusindika vyakula mbalimbali na matunda.
Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa SIDO mkoa wa Dodoma bw, Twaha Swed amesema wahitimu hao wanatarajia kupatiwa Mashine mbalimbali ili kuanza kufanya kazi.
Akijibu Risala ya WAUVI Mgeni Rasmi Bi Fatma Toufiq ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge, ya masuala ya ustawi na maendeleo ya jamii ambaye pia ni mbunge Viti maalumu mkoa wa Dodoma, amesema atawasilisha ombi lao kwa Mkurugenzi wa jiji, la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda kikubwa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAUVI mkoa wa Dodoma akamuomba mgeni rasim kusaidia upatikanaji wa mikopo huku baadhi ya wahitimu wakiomba mikopo hiyo itolewe kwa wakati.