Ubuyu ni fursa kwa wafanyabiashara
21 March 2023, 6:12 pm
Kwa mujibu wa wa wataalamu wa afya ubuyu ni tunda jamii ya adonsonia ambapo umekuwa na matumizi mbalimbali kwani wapo baadhi yao hutumia kama juisi na wengine huongezea thamani kwa kutengenezea bidhaa mathalani kashata au ubuyu wa rangi.
Na Thadei Tesha.
Ubuyu ni miongoni mwa bidhaa inayopatikana katika jiji la Dodoma ambapo pia imetoa fursa kwa watu kujipatia kipato pale wanapoongeza thamani bidhaa hiyo.
Dodoma tv imepita sokoni na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa hiyo ambapo wanasema mbali na bidhaa hiyo kuwa na changamoto katika upatikanaji wake kipindi cha mvua lakini imekuwa na umuhimu mkubwa kama wanavyobainisha.
lakini je ni bidhaa gani zinazoweza kuzalishwa pale zao hili linapoongezewa thamani?