Wananchi kulipwa fidia ya bilioni 10 kupisha ujenzi wa barabara Ntyuka
17 March 2023, 4:34 pm
Barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami inagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 38 na hadi kufikia mwezi Feburuary ujenzi umefikia asilimia 4.
Na Mindi Joseph.
Jumla ya wananchi 1522 Mkoani Dodoma wanatarajiwa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 10 ili kupisha Ujenzi wa Barabara ya Ntyuka Mvumi hadi Kikombo yenye urefu wa kilometer 25.
Ameyasema hayo jijini Dodoma Mkuu wa matengenezo TANROAD Mhandisi Salome Kabunda wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023.
Kwa uapnde wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amehimiza ufuatiliaji wa barabara ya Mpunguzi.
Naye Mbunge wa Bahi Mh Keneth Nollo amesema milion 900 zinatumiaka katika ujenzi wa barabara ya Mpunguzi.
Kikao cha Bodi ya Barabara kimefanyika leo jijini Dodoma kikiwakutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kujadili utekeleza wa bajeti ya mwaka 2023