CDF lasaidia kupunguza mimba za utotoni Mpwapwa
8 February 2021, 1:43 pm
Na,Mindi Joseph,
Dodoma.
Zaidi ya wanafunzi elfu moja kutoka shule 8 za Sekondari na 12 za Msingi Wilayani Mpwapwa, wamefanikiwa kupata mafunzo ya kuwajengea mazingira salama wawapo shuleni toka mwaka 2017.
Akizungumza na Taswira ya habari meneja miradi kutoka Shirika la Jukwaa la utu wa Mtoto (CDF), Evans Antony amebainisha kuwa tangu walipoanzisha mradi wa uwezeshaji watoto na ushiriki wa jamii katika kujenga mazingira salama yasiyo na ukatili Wilayani humo, wamefanikiwa kupunguza mimba za utotoni kwa wanafunzi.
Katika hatua nyingine Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka katika shule nne za Sekondari Wilayani Mpwapwa ambao wamesema mafunzo hayo yamechangia kuwanusuru na changamoto zinazokatiza ndoto zao.
Kwa upande wake Mwalim Paskazia Kajuna kutoka shule ya Sekondari Ihala pamoja na mwalimu Timoth Timoth kutoka shule za Msingi Mtejeta, wamesema Shirika la utu wa Mtoto CDF limekuwa mdau mkubwa katika kuhakikisha linawajengea mazingira salama wanafunzi shuleni.