nyumba 150 za watumishi umma zimeanza kujengwa eneo la nzuguni
26 November 2021, 1:53 pm
Na;Mindi Joseph .
Jumla ya nyumba 150 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni zimeanza kujenga kupitia Miradi inayotekelezwa na wakala wa majengo Tanzania TBA jijini Dodoma huku zikitarajiwa kukamilika mwezi June 2022.
Akizungumza katika Ziara ya viongozi wa Wizara ya Nyumba na maendeleo ya makazi SMZ na wakala wa majengo zanzibar ZBA Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki [TBA] Said Mndeme amesema mradi huo mkubwa wa ujenzi wa jumla ya nyumba 3500 ambapo 150 zimeanza kujengwa wamejipanga kuhakikisha mahitaji yote ya ujenzi yanakuwepo ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Ameongeza kuwa mbali na ujenzi wa nyumba za watumishi wanatekeleza ujenzi wa nyumba 20 za viongozi katika eneo la Kisasa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi (SMZ) Joseph Kilangi ameishukuru TBA kwa ziara hiyo ambayo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya zanzibar na Tanzania na kuona kazi zinazofanywa na wakala wa majengo tanzania.
Naye Eng. Kassim Omar Kaimu Mkurugenzi Wakala wa majengo Zanzibar ZBA amesema wamejifunza na kuona kupitia miradi wanayoitekeleza ya ujenzi wa nyumba za watumishi na viongozi zilizo katika kiwango bora.
Zaidi ya Sh Bilion 12 zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 150 katika eneo la Nzuguni lenye ukubwa wa Ekari 630 huku bilioni 7 zikitolewa kwaa ajili ya kuanza ujenzi huo na zaidi ya bilion 5 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi katika kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi wa umma.