Wakazi wa Mkoka walalamikia tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara
3 September 2021, 1:15 pm
Na ;Victor Chigwada.
Changamoto ya kukatika kwa umeme pamoja na uhafifu wa upatikana wa huduma hiyo katika Kata ya mkoka Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma umeelezwa kuchangia kushusha uchumi wa wananchi kwa ujumla.
Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa Mkoka ni moja ya maeneo yanayo jiendesha kwa shughuli za viwanda vidogo vidogo lakini kukosekana kwa umeme wa uhakikika unadidimiza uchumi huo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mkoka Bw. Elia Chibago amekiri kuwepo kwa changamoto ya kukatika mara kwa mara huduma ya umeme na imekuwa ikichangia kuwaathiri wananchi wanaoendesha shughuli za viwanda vidogo vidogo huku baadhi ya maeneo yakiwa hayajafikiwa na huduma hiyo
Naye Diwani wa Kata hiyo Bw. Richard Mwite ameeleza kukabiliwa na changamoto hiyo licha ya sasa TANESCO kuanza kushughulikia tatizo hilo ambalo itakuwa ahueni kwa watu waliojikita katika shughuli za kiuchum kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.