Dodoma FM

Wakazi wa Msanga walalamikia uchakavu wa barabara unao sababishwa na magari makubwa

18 August 2021, 2:02 pm

Na; Victor Chigwada.


Wa
nanchi wa Kata ya Msanga Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wamelalamikia uchakavua wa barabara unao sababishwa na magari makubwa yanayobeba madini ya mchanga katika kijiji cha msanga.

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema licha ya makusanyo ya kodi katika safari za magari hayo lakini bado barabara hiyo imeendelea kuwa chakavu na kugeuka changamoto kubwa kwa wananchi

Mwenyekiti wa Kijiji cha Msanga Bw. Hatibu Ramadhani amekiri ubovu wa barabara hiyo kuwa adha kwa wananchi licha ya Hamashauri kukusanywa mapato katika uchimbaji huo wa madini ya mchanga

Diwani wa Kata hiyo Bw. Emmanueli Ng’hata amesema uchakavu wa barabara hiyo unachangiwa na magari yanayobeba madini ya mchanga na tayari wanaendelea na mikakati kwa ajili ya marekebisho kupitia Halmashauri

I

Ukusanyaji wa mapato Nchini kupitia Halmashauri umekuwa ukisaidia kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwa ni pamoja na urekebishaji wa miundombinu, ikiwemo sekta ya elimu, afya pamoja na uchimbaji wa visima vya maji.