Wakazi wa mtaa wa Mkoyo wametakiwa kuzingatia bei halali ya uingizaji wa umeme
12 July 2021, 12:32 pm
Na; Benard Filbert.
Wakazi wa mtaa wa Mkoyo kata ya Hombolo Jijini Dodoma waeombwa kuzingatia bei halali ya uingizaji wa umeme wa REA ambayo ni elf 27 na sio vinginevyo.
Tahadhari hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Hombolo Bw. Ased Mathayo wakati akizungumza na Taswira habari ambapo amewataka wananchi wa kata hiyo kutokukubali kurubuniwa na mtu yeyete kwani bei elekezi kutoka Serikalini ni elf 27 tu.
Ameongeza kuwa kupitia gharama hiyo inahusisha kila kitu ikiwemo nguzo ambazo zitakuwa zikielekezwa kila nyumba yenye uhitaji.
Akizungumzia maendeleo ya shughuli hiyo amesema hivi sasa wanakaribia kuanza kuweka nguzo hususani maeneo yote ambayo hayakuwahi kuwa na nguzo hizo.
Mmoja wa wakazi wa Kata hiyo Bw. Fidelis amesema kuja kwa umeme utasaidia kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi kutokana na Kata hiyo kuwa kinala katika kilimo cha mazao ya biashara.
Upatikanaji wa nishati ya umeme huchochea kukuza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi wakiwemo wale wanaoishi maeneo ya vijijini kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo.