Wazazi wakiri uwepo wa dhana tofauti na uelewa mdogo katika maswala ya hedhi
28 May 2021, 1:54 pm
Na;Yussuph Hans.
Ikiwa leo ni siku ya hedhi Duniani moja ya changamoto wanayokutanayo wasichana nchini, ni baadhi ya wazazi kushindwa kubadili mtazamo wao na kuvunja ukimya kuhusu masuala ya hedhi.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya Wasichana jijini hapa wakati wakizungumza na taswira ya habari juu ya changamoto walizopitia katika kipindi cha hedhi.
Scola Is-Haka na Saudat Saidi wamesema kuwa hedhi yao ya kwanza ilikuwa na changamoto kubwa, ambapo tofuati na Glory Martin yeye Elimu ya hedhi aliipata kutoka kwa wazazi wake na ilimsaidia kwa kiasi kikubwa kuikabili hali hiyo.
Kwa upande wao Wazazi wamekiri kuwepo kwa uelewa mdogo kuhusu masuala ya hedhi huku baadhi yao wakichukulia hali hiyo kama dhana tofauti.
Naye Afisa Programu kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Jackson Malangalila amesema kuwa suala la hedhi limekuwa likihusishwa na imani tofauti katika baadhi ya jamii hali inayoweza kuathiri afya ya msichana.
Siku ya hedhi Salama huadhimishwa kila mwaka ifikapo Mei 28, ikiwa na lengo la kuleta pamoja sauti za Wadau mbalimbali ili kuhamasisha hedhi Salama kwa Wasichana na Wanawake.