Jamii yatakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo yakuambukizwa
11 May 2021, 12:40 pm
Na; Mariam Matundu.
Jamii imetakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa ikiwemo Covid 19 ili kulinda afya zao .
Hayo yamesemwa na afisa afya wa jiji la Dodoma Abdallah Mahiya na kuongeza kuwa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 kuendelea kuwepo katika nchi za nje hapa nchini Tanzania hakuna budi kuendelea kuzingatika miongozo ya wataalamu wa afya katika kuchukua tahadhali.
Aidha amesema jiji la Dodoma limewaelekeza watendaji katika ngazi za mtaa na Kata kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu na kuhakikisha tahadhali zote zinachukuliwa ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara.
Kuhusu matumizi ya tiba asili Bw.Mahiya amesema ni muhimu kutumia tiba asili katika kujikinga na magonjwa ikiwemo kujifukiza kwa kufuata ushauri na miongozo ya wataalamu wa afya katika kutumia tiba hizo.
Ugonjwa wa Covid-19 umeendelea kuleta madhara makubwa katika nchi mbalimbali tangu ulipolipuka mwaka 2019 huko nchini China.