Dodoma FM

Zifahamu fursa na changamoto za msichana kielimu

12 November 2024, 5:27 pm

Na Fred Cheti.                                              

Idadi ya wanafunzi wasichana wanaomaliza kidato cha nne imetajwa kuongezeka licha ya vikwazo vingi vinavyowakabili katika safari ya kielimu.

Hii imebainika katika mtihani wa kuhitimu kidato cha nne uliofanyika Novemba 11, 2024  ambapo idadi ya wasichana waliofanya mtihani  wa kuhitimu kidato cha nne imetajwa kuwa kubwa tofauti na  wavulana.

CLIP 1…….KATIBU MTENDAJI BARAZA LA MITIHANI NECTA

Mkuu wa kitengo cha tathimini Bwn. Fransis Shayo kutoka shirika la Msichana Initiative anaelezea fursa ambazo msichana anazoweza kuzipata kwa kuhitimuhitimu kidato cha nne pia anabainisha vikwazo ambavyo wanafunzi wasichana wamekuwa wakipitia katika safari yao ya kielimu.

Pichani Mkuu wa kitengo cha tathimini Bwn. Fransis Shayo kutoka shirika la Msichana Initiative
Sauti ya Bwn. Fransis Shayo

Katika kuhakikisha msichana anabiliana na changamoto mbalimbali ili kufikia malengo yao ya kielimu waalimu ni moja ya kundi muhimu katika kutimiza ndoto za wasichana kielimu kama anavyoeleza Mwl. Rahma Saidi Mlezi wa Klabu ya wasichana kutoka Msicana Intiative.

Pichani Mwl. Rahma Saidi Mlezi wa Klabu ya wasichana kutoka Msicana Intiative.
Sauti ya Mwl. Rahma Saidi

Ripoti iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, lile la masuala ya wanawake, UN-Women na shirika pamoja na Plan International, inaonesha kuwa idadi ya wasichana wanaoandikishwa shule na kuhitimu masomo ni kubwa kuliko wakati wowote. Aidha idadi ya wasichana watoro shuleni  imepingua kwa kiasi kikubwa toka mwaka 1995.