Zuia magonjwa yasiyoambukiza kwa kuchangia damu
12 November 2024, 10:23 am
Na Anwary Shabani.
Wananchi wametakiwa kujenga utamaduni wa kujitokeza kuchangia damu ili kusaidia kuzuia magonjwa yasiyoamabukiza.
Mratibu wa damu salama katika jiji la Dodoma Jerome Felician ameyasema hayo wakati wa kampeni ya uchangiaji damu inayojulikana kama “ Zuia Magonjwa Yasiyo Ambukiza Kwa Kuchangia Damu” iliyofanyika Nov. 09, 2024 katika viwanja vya Nyerere Squire.
Aidha Bwn. Christopher Mkano ambaye ni mtaalamu wa afya kutoka Dodoma amezungumzia umuhimu wa mwananchi kuchangia damu salama.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu walikuwa na haya ya kusema
Sanjari na hayo Mratibu huyo amewatoa hofu wananchi juu ya suala la uchangiaji damu kuwa halina tatizo lolote hivyo wasiogope kwenda kuchangia damu