Msimu wa kilimo wazinduliwa Singida
6 November 2024, 5:53 pm
Na. Anselima Komba
Wakulima Mkoani Singida wametakiwa kujiandikisha katika daftari la ruzuku ya mbolea ili kufaamu kawango cha mbolea kinachohitajika katika msimu huu wa kilimo.
Hayo yamejiri wakati Mkuu wa Idara maendeleo ya Jamii Francis Mashallo Akizindua Msimu wa Kilimo 2024/2025 kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Mhe.Godwin Gondwe .
Aidha Diwani kata ya Ilongelo Issa Mwiru amewataka wakulima kuwekeza zaidi katika kilimo hili kujikwamua na umasikini.
Pia Afisa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Nathalia Mosha amesema lengo kuu la uzinduzi wa msimu wa kilimo ni kutoa uhabarisho kwa wakulima juu ya kuanza kwa msimu wa shughuli za kilimo katika Halimashauri pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la ruzuku ya mbolea ili wapate namba ambayo itatumika kununua Mbolea .
Sambamba na hilo Mhandisi wa Kilimo Bwn. Shani Selemani anaelezea mchakato wa upimaji na mahitaji ya udongo katika kilimo.