Upungufu wa vituo vya huduma ya Afya ya uzazi kwa vijana warudisha nyuma mapambano dhidi ya ukimwi
29 April 2021, 2:50 pm
Na; Mariam Matundu.
Upungufu wa vituo vinavyotoa huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana umetajwa kuwa moja ya changamoto inayorudisha nyuma mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi .
hayo yamesemwa na Rosemary Shani balozi wa wasichana balehe wakati akisomaa risala katika uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za vvu na UKIMWI zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana .
aidha ameiomba serikali kupanua wigo wa kutoa elimu na umuhimu wa afua za vvu na UKIMWI kwa wasichana balehe na wanawake vijana.
Nae mgeni rasmi katika uzinduzi huo naibu waziri wa kazi mh Patrobasi Katambi amesema serikali imeweka kibaumbele katika mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi ambapo katika bajeti ya kila wizara ni lazima kulitazama suala la ukimwi,pamoja na mbio za mwenge lazima ziwe na ujumbe wa mapambano dhidi ya vvu na UKIMWI.
Mh katambi amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuwalinda wasichana balehe kwa kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Wadau mbalimbali wanaotekeleza afua za vvu na UKIMWI zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana wamekutana leo katika mkutano wa mwaka unaofanyika kwa siku mbili ukiwa na kauli mbiu PAMOJA HAINA KUFELI.