Dodoma FM
Je sheria inasemaje umiliki wa mali binafsi katika ndoa?
29 October 2024, 8:05 pm
Na Leonard Mwacha.
Suala la umiliki wa mali binafsi katika ndoa limekuwa na sintofahamu kutokana na kukosekana kwa elimu ya umiliki wa mali kwa wanandoa.
Hali hiyo huweza kuleta changamoto za mahusiano baina ya wanandoa haswa pindi ambapo mali hizo humilikiwa kwa siri licha ya sheria kuruhusu wenza kumiliki mali binafsi.
Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Euphrasia Peragiusan afafanua zaidi juu ya sheria ya umiliki wa mali binafsi katika ndoa.