Dodoma FM
Jipime mwenyewe VVU kwa mate yako
24 October 2024, 7:49 pm
Na Mindi Joseph.
Huduma ya kipimo cha virusi vya ukimwi cha kujipima mwenyewe kwa kutumia mate imeanza kutolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Dkt Adam Adam Mhudumu wa afya ngazi ya jamii anaelezea namna ya kutumia kipimo hicho.
Msimamizi wa Kitengo cha tiba na matunzo Bi. Zainabu Nashombwa ameshauri jamii kupima afya zao ili kuepuka magonjwa nyemelezi endapo watabaika kupata maambukizi ya VVU.