Senyamule aagiza mkandarasi kukamilisha miradi
23 October 2024, 7:00 pm
Na Mindi Joseph.
Wasimamizi wa miradi ya maendeleo hususan Shule, wametakiwa kusimamia na kukamilisha miradi kwa wakati kwa kutumia mfumo wa manunuzi Serikalini (NeST).
Wito huo umetolewa na Mhe. Rosemary Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika ziara ya ukaguzi wa miradi jijini Dodoma Oktoba 21, 2024, ambapo alitembelea miradi ya madarasa, shule mpya na nyumba za walimu katika shule za Sekondari Mpunguzi, Matumbulu na Miyuji ‘B’.
Imebainika kuwa miradi ya shule hizo imeonekana kuwa nyuma ya wakati huku sababu zikitolewa kuwa ni changamoto zilizojitokeza kwenye matumizi ya mfumo wa NeST hivyo, Mhe. Senyamule alitoa ufafanuzi;
Ziara hiyo ilianzia kwenye shule ya Sekondari ya Mpunguzi ambayo imetekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa matatu na matundu nane (08) ya vyoo kwa kiasi cha shilingi 83,400,000/= fedha kutoka Serikali kuu na mradi huo umekamilika kwa asilimia 95.