Dodoma FM

Uthubutu kikwazo vijana kuwania nafasi za uongozi

21 October 2024, 7:34 pm

Na Anwary Shabani.                                               

Uthubutu na hofu vimetajwa kuwa kikwazo kwa vijana  kuwania nafasi  za uongozi kuanzia ngazi za serikali za mtaa.

Jofrey Regnand Mtasiwa kutoka katika tasisi ya  Kijana Foundation jijini Dodoma amebainisha kuwepo kwa hofu na kutokuthubutu  miongoni mwa vijana katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Pichani Jofrey Regnand Mtasiwa kutoka katika tasisi ya  Kijana Foundation jijini Dodoma
Sauti ya Bwn. Jofrey Regnand Mtasiwa

Baadhi ya vijana jijini Dodoma wamesema  kukosekana kwa msingi  imara  wa malezi ya uongozi toka katika ngazi ya familia imechangia vijana kukwama katika kugombea nafasi mbalimbali.

Pichani kijana akielezea vikwazo vinavyowakanili kuwania nafasi za uongozi
Sauti za vijana
Pichani kijana akielezea vikwazo vinavyowakanili kuwania nafasi za uongozi

Aidha Jofrey Mtasiwa amewashauri vijana waweze kushiriki katika kazi mbalimbali za kijamii ili wananchi waweze kuwaamini.

Sauti ya Bwn. Jofrey Regnand Mtasiwa