Dodoma FM

MPWUWSA yakutana na wananchi kujadili kero za maji

15 October 2024, 7:29 pm

Na Noel Steven

Mamlaka ya maji safi Mpwapwa (MPWUWSA) imekutana na wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa katika wiki ya huduma kwa mteja kujadili kero za maji zinzoawakabili wananchi kwa sasa.

Katika kikao hicho ,  wananchi wameishauri mamlaka hiyo kufanya ukarabati wa chanzo cha Mayawile ili kuweza kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wengi zaidi.  

Pichani watendaji wa MPWUWSA katka kikao na wananchi kujadili kero ya maji
Sauti za wananchi

Aidha Bi. Habiba Kidunda Meneja huduma kwa wateja MPWUWSA ameeleza changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo katika kutoa huduma kwa wananchi ni pamoja na uchepushaji wa maji kinyume na utaratibu kwa baadhi ya wananchi.

Pichani Bi. Habiba Kidunda meneja huduma kwa wateja
Sauti ya Bi. Habiba Kidunda