Dodoma FM

Mwalimu atiwa mbaroni kwa tuhuma za ubakaji

14 October 2024, 7:58 pm

Na Mindi Joseph.

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limefanikiwa kumtia nguvuni mwalimu ambaye ni mtuhumiwa wa ubakaji na amefikishwa mahakamani kujibu tuhumu zinazomkabili.

Tukio hilo la ubakaji limetokea katika kijiji cha Nhinhi kilichopo umbali wa Km 50 kutoka ndani ya Jiji la Dodoma ambapo mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) amekiri kubakwa na mwalimu na kutishia kuuwawa endapo angetoa siri hiyo kwa watu.

Pichani Kijiji cha Nhinhi jijini Dodoma
Sauti ya mwanafunzi

Aidha mwenyekiti wa kijiji cha Nhinhi jijini Dodoma Asa Joseph amewataka wazazi kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa watoto mara tu wanapobaini kutokea au kuwepo kiashiria cha kutokea ili hatua zichukuliwe kwa wakati.

Pichani Mwenyekiti wa kijiji cha Nhinhi jijini Dodoma Asa Joseph
Sauti ya Bwn. Asa Joseph