Dodoma FM
Babu adaiwa kumlawiti mjukuu wake na kutoweka
7 October 2024, 7:03 pm
Na Mindi Joseph.
Babu anayedaiwa kumlawiti mjukuu wake wa miaka 12 katika Mtaa Ipagala jijini Dodoma ametoweka nyumbani kwake na hajulikani alipo baada ya kufanya tukio hilo mwishoni mwa wiki jana.
Mwenyekiti wa mtaa wa Ipagala jijini Dodoma Bw. Elenei Paulo amesema kuwa walipata taarifa hiyo kutoka kwa walimu wa shule anayosoma binti huyo.
Baadhi ya majirani ambao wanamfahamu kwa ukaribu babu huyo wameshangazwa na kitendo alichofanya mzee huyo . Tukio hilo limetokea mwishoni wa wiki jana na kuzua sintofahamu katika jamii.