Dodoma FM

Elimu ya uongozi shuleni ni chachu kwa wasichana kuwania nafasi za uongozi

4 October 2024, 8:09 pm

Na Mindi Joseph.

Elimu ya uongozi kwa wanafunzi inawasaidia kujitambua kujiamini na na kuwajengea ari ya kuwa viongozi  kwa siku za baadaye.

Mwalimu Winfrida Maliga anasema elimu hiyo inawasaidia wanafunzi kutambua umuhimu wa kuwa viongozi wakiwa shuleni hata wakiwa katika jamii.

Mwalimu Winfrida Maliga
Sauti ya Mwalimu Winfrida Maliga

Jitihada za Shirika la Msichana Initiative zimeendelea kupambana na changamoto ya mila potofu zinazoonekana kukwamisha wasichana  kupata elimu ya uongozi  itakayowajegea ari ya kugombea nafasi za uogozi siku za baadae kama anavyobainisha Tumaini Godwine.

Pichani Tumaini Godwine kutoka Shirika la Msichana Initiative

Aidha wanafunzi wa shule ya Kipanga Sekondari na Msingi wanasema elimu ya uongozi ni nguzo kwao ya kupiga vitendo vinavyofanyika na jamii kumdidimiza msichana.

Sauti za wanafunzi wasichana