Dodoma FM

Bashungwa amnyoshea kidole Mkandarasi Dodoma

4 October 2024, 8:09 pm

Na Fredi Cheti

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na usimamizi wa barabara ya mzunguko wa nje ya jiji la Dodoma (Dodoma Ring Road ) kwa kiwango cha lami na kumtaka Mkandarasi Kampuni ya AVIC kuwasilisha mpango kazi utakaomuwezesha kukamilisha ujenzi ifikapo mwezi Machi, 2025.

Bashungwa ametoa agizo hilo wakati akikagua ujenzi  wa mradi ambapo amesisitiza Mkandarasi huyo kuongeza nguvu kazi, mitambo na kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba.

Waziri wa Wizara ya Ujenzi Innocent Bashungwa akiwa na Mkandarasi wa ujenzi mradi
Sauti ya Innocent Basgungwa Waziri w Ujenxi

Katika hatua nyingine waziri Bashungwa amsema Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi hasa ya barabara na madaraja katika maeneo mbalimbali nchini itakayofungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi.

Pichani uhenzi wa barabara ya mzunguko ukiendelea

Aidha Waziri Basungwa ametoa magizo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya ujenzi kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma.

Pichani sehemu ya barabara ya mzu guko
Waziri Innocent Bashunjhwa akitoa maagizo ya usimamiaji wa ujenzi wa barabara za mzunguko