Dodoma FM

Gharama za umeme ni kikwazo cha maendeleo kiuchumi Ng’ong’ona

17 September 2024, 9:00 pm

Licha ya jitihahada za Wakala umeme Vijijini (REA) kusambaza huduma ya umeme katika vijiji takribani 12,318 , wananchi wa Mtaa wa Ng’ong’ona Jijini Dodoma wamedai kuwa gharama ya kuvuta umeme kwa sasa ni kubwa

Na  Mindi Joseph.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea kuwezesha upatikanaji wa nishati bora maeneo ya vijijini ili kuimarisha maisha ya wananchi kwa kuibua fursa ya shughuli za kiuchumi kama anavyoeoeleza  Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy anafafanua Zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy
Sauti Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy

Licha ya jitihahada hizo, Wananchi wa Mtaa wa Ng’ong’ona Jijini Dodoma wamedai kuwa gharama ya kuvuta umeme kwa sasa ni kubwa hivyo imechangia wengi wao kujikuta wakikosa huduma hiyo kusababisha kuwa duni kiuchumi kwa kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi. 

Picha ya moja ya mkazi wa Ng’ong’ona akizungumzia juu ya gharama za umeme
Sauti za wananchi
Picha kuonesha miundombinu ya umeme

Wakala wa Nishati Vijijini imekamilisha kufikisha umeme vijiji vyote na sasa imeanza upelekaji umeme katika vitongoji 3,060 nchini.