Wakazi Dodoma wajawa shauku maonesho ya nanenane
31 July 2024, 7:30 pm
Maonesho hayo huanza tarehe 01 hadi 08 ya mwezi Agosti. Maonesho hayo huambatana na uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia bora za kilimo, ufugaji na uvuvi.
Na Fred Cheti.
Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Ufugaji (Nanenane) yanatarajia kuanza rasmi siku ya kesho Agosti 1 huku wakazi wa Dodoma wakiwa na shauku kubwa ya kuona maonesho hayo.
Maonesho hayo huchukua Watu wengi kutoka kila kona ya Mkoa wa Dodoma mwaka huku yakitarajiwa kukutanisha Watu wengi zaidi kutokana na kufanyika Kitaifa ambapo wakazi wa Dodoma wakiwemo Wajasirimali wakisubiri kwa hamu kuiishi Msemo usemao” Mgeni aje Mwenyeji apone” kutokana na fursa nyingi hasa kiuchumi zitokanazo na maonesho hayo.
Kwa asilimia kubwa maandalizi ya maonesho hayo yanatarajiwa kuwa na utofauti mkubwa na maonesho yaliyopita kama ambavyo anabainisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.
Kila Mwaka kuanzia tarehe 01 hadi 08 ya Mwezi Agosti. Maonesho hayo huambatana na uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia bora za kilimo, ufugaji na uvuvi. Pia, maonesho hayo hushirikisha Wadau mbalimbali zikiwemo Wizara, Taasisi za Umma na Binafsi, Wabia wa maendeleo, Wakulima na Vyama vya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi.