Vumbi lahatarisha afya za wakazi Miganga
31 July 2024, 6:52 pm
Eneo hili la Miganga lipo mita 600 tu kutoka stesheni ya SGR, je, serikali haioni changamoto hii na kuwasaidia wananchi hawa ambao wanaona wametelekezwa?.
Na Mindi Joseph.
Wakazi mtaa wa Miganga wamelalamika kuathirika kiafya kutokana na adha ya vumbi inayosabishwa na kubomolewa kwa barabara kwa ajili ya ujenzi wa daraja la SGR.
Matumaini yamepotea kwa wakazi hao ambao wamezungumza na Dodoma TV wanasema serikali imeshindwa kuwajengea kipande hicho kwa kiwango cha lami na wao kuendelea kuathirika kiafya kwa kuugua vifua na macho.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miganga Ludovick Chogwe anasema pamoja na jitihada za kufika mamlaka husika Tanroad na upande wa SGR hakuna kinachofanyika.
Je, vumbi lililochangannywa na saruji lina athari gani kwa afya ya binadamu? Dkt. Damas James kutoka Hospital ya St. Livingstone anaeleza.
Nini hatima ya wananchi hawa licha ya Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa kufika eneo hilo na kutaka Tanroad na SGR kukaa meza moja lakini imeshindikana?.