Dodoma FM
Ufahamu umuhimu wa Nyuki katika mazingira
18 May 2024, 6:53 pm
Wananchi wanaaswa kuendelea kutunza mazingira pamoja na kujihusisha na ufugaji wa nyuki kwani ni fursa itakayo wakwamua kiuchumi.
Na Mariam Kasawa.
Nyuki anatajwa kuwa mdudu muhimu sana katika Afya na mazingira kwani viumbe hai wote wanategemea uchavushaji wa nyuki kujipatia chakula na matunda.
Akiongea na Dodoma Tv Mtafiti kutoka TAWIRI Kipemba Ntiniwa anasema nyuki anafaidi nyingi katika mazingira kwani uchavushaji wake unafaida sana kwa viumbe hai.
Aidha bw. Kipemba ameyataja makundi ya nyuki katika mzinga na majukumu yao katika uzalishaji wa asali.