Dodoma FM

Wanafunzi Kongwa wajifelisha mitihani kwa ajili ya kazi za ndani

7 May 2024, 6:41 pm

Picha ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw, White Zuberi akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka.Picha na Alfred Bulahya.

Wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wamekuwa wakishindwa kuhitimu masomo yao.

Na Alfred Bulahya.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kongwa mkoani Dodoma wamekuwa wakishindwa kuhitimu masomo yao huku wengine wakijaza majibu ya uongo kwenye mithani yao ya mwisho ili waende kufanya kazi za ndani.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw, White Zuberi wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka.

Sauti ya Bw, White Zuberi.
Picha ni kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka.Picha na Alfred Bulahya.

Akimwakilisha Katibu tawala wa mkoa wa Dodoma ….amesema ili kuondoa changamoto hizo ni kuanza kudhibiti utoro na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni.

Sauti ya Mwakilishi wa katibu Tawala.

Nao baadhi ya Madiwani wilayani humo wakawa na haya ya kusema